COME AND SEE Header Animation
COME AND SEE ANIMATED HEADER
WIMBO WA UPENDO NKONE WA HALELUYA AKIWA COLUMBUS U.S.A
Wednesday, September 11, 2013
Tuesday, March 19, 2013
GOSPEL IN AFRICA: Africori director Mr. Kenan Zim to Sign Online Dea...
GOSPEL IN AFRICA: Africori director Mr. Kenan Zim to Sign Online Dea...: Africori Boss Mr. Yoel Kenan FORMER Europe Sony Records vice p...
Monday, March 4, 2013
KARIBU KWEYE TAMASHA LA KIHISTORIA LILOWAKUSANYA WAIMBAJI WAKONGWE WA ZAMANI TAREHE 17/3/2013 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE
lile tamasha la kihistori ambalo limewakusanya waimbaji binafsi , kwaya na Band kongwe sasa zimebakia wiki mbili kuweza kufanyika ni tarehe 17/3/2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni , watu na wadau wa muziki wa injili wanaombwa waipitwe na tukio jili muhimu wajitokeze kwa wingi kuwapa ushirikiano waimbaji wetu wa zamani. Come and see promoters inawaomba wale wote wenye blog zao kuweza kusaidia kulitangaza Tamasha hili ili watanzania na wadau wa muziki wa injili wasipitwe na tukio hili muhimu.
MFANO WA TUZO ITAKATOTOLEWA KWA WAKONGWE WA MUZIKI WA INJILI
GOGE JABILI KIONGOZI WA LULU KWAYA ATAONGOZA SAFU YA KWAYA YAKE
MARTINI UBWE MOJA YA MASOUND ENGINER WA TAMASHA
Monday, February 25, 2013
WAIMBAJI WAKONGWE WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA WAJIPANGA WAINGIA KAMBINI
Waimbaji wa muziki wa injili Tanzania Charles Jangarasoni, Mzungu four, Masaga nyanda,Efrahimu mwasasu sasa waingia kambini kujifua kwajili ya Tamasha kubwa la wakongwe wamuziki wa injili Tazania , wakiongea kwa nyakati tofauti na mratibu wa Tamasha hili Bwana Emmanuel Ezekiel, Wamesema kuwa Mungu atashuka siku hiyo kwa kuwa wameanza maombi ya kufunga na kuomba kwajili ya kuliombea Tamasha hili la kipekee, Na wameahidi kuwa watanzania watarajie vitu vya tofauti ambavyo walikuwa wamevimisi kutoka kwako.Tamasha litazinduliwa rasmi tarehe 17/3/2013 katika ukumbi wa diamond jubilee.Mara baada ya uzinduzi wa tamasha hili litaelekea mkoa wa Arusha , Mwanza, Mbeya Iringa Dodoma, Singida,Kigoma, Tabora na Mtwara na litakuwa likifanyika kila mwaka likijumuisha wakongwe pekee wa muziki wa injili Tanzania.
Askofu Charles Jangarasoni mmoja ya waimbaji watakohudumu
Nathaniel Hingi toka Moshii
Mchungaji Mzungu Four
Askofu Jangarason
Mchungaji Ency Mwalukasa
Pastor Safari
MUIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI UPENDO KIRAHILO NA AMONI KILAHILO SASA KUSHILIKI KATIKA TAMASHA KUBWA LA WAKONGWE WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA
Jumapili hii mratibu mkuu na muandaaji wa Tamasha la Wakongwe wa muziki wa injili Tanzania bwana Emmanuel Ezekiel ( Pastor Pepea ), alifanya kikao kikubwa na Amoni na Upendo kirahilo jumapili hii na kukubali kushiliki katika Tamasha kubwa la kuwaenzi wakongwe wa muziki wa injili Tanzania. Amoni na Upendo kirahilo ni moja ya waimbaji wakongwe watakao lishambulia jukwaa la Tamasha la wakongwe wa muziki wa injili Tanzani. Tamasha hili linatarajia kufanyika tarehe 17 March 2013 katika ukumbi mkubwa wa Diamond Jubilee kunzia saa 8:00 mchana hadin saa 12:00jioni.Katika Tamasha hili kunatarijiwa kutolewa tuzo za heshima ili kutambua mchango wao mkubwa walioutoa katika kuinua na kuendeleza muziki wa injili Tanzania.Upendo na Amoni kirahilo wamewaomba watanzania wote, wadau wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia kile ambacho wakongwe wa muziki wa injili wamekiandaa kwajili yao.
UPENDO KIRAHILO
Upendokirahilo katika moja ya huduma zake.
Upendo kirahilo
Upendo Kirahilo
Upendo Kirahilo
Upendo kirahilo katika moja ya huduma zake.
Upendo kirahilo ameahidi kufanya onyesho la nguvu na kudhihilisha kuwa yeye ni mkongwe katika muziki wa injili. Upendo alianza kuimba akiwa bado ni binti mdogo, amewataka waimbaji wachanga kuja kujifunza kutoka kwa wakongwe wa muziki wa injili kama wanataka kuendelea kufanya vizuri katika mziki wao na kudumu kwa mda mrefu.
Saturday, February 23, 2013
TAMASHA LA WAKONGWE WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA MAANDALIZI YAPAMBA MOTO
Kampuni ya COME AND SEE PROMOTERS imeandaa Tamasha kubwa la wakongwe wa muziki wa injili Tanzania kwa lengo la kutambua mchango mkubwa ambao wameutoa waimbaji hawa wazamani wa muziki wa injili katika kuinua na kuendeleza mziki wa injili Tanzania. Akiongea kwa nyakati tofauti mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Come and see Promoters bwana Emmanuel Ezekiel ( Pastor Pepea ) Amesema hili ni tamasha la kihistori ambapo halijawahi kutokea katika nchi yetu ambapo waimbaji wote wakongwe wa mziki wa injili kukutana katika jukwaa moja.Tamasha hili limepewa jina la OLD IS GOLD DAY linatarajia kufanyika tarehe 17/3/2013 katika ukumbi mtulivu wa Diamond Jubilee kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni na kukusanya wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikari,viongozi wa dini, waandishi wa habali nk.
Tamasha hili litaambatana na utoaji wa Tuzo za heshima kwa waimbaji hawa wakongwe ili kutambua mchago wao katika kuinua na kuendeleza wa injili Tanzania. Waimbaji wakongwe wa mziki wa injili watakaoshambulia jukwaa ni MZUNGU FOUR, JANGARASONI, MASAGA NYANDA,DAVIDI NKONE, NATHANIEL HINGI, MWASASU, MWASUMBI, ENCY MWALUKASA, AMON NA UPENDO KIRAHIRO, NEW LIFE BAND TOKA ARUSHA, na kwa upande wa kwa ya ni LULU KWAYA NAYOTH KWAYA ,VICTORY SINGERS , MSASANI KWAYA NK na kusindikizwa na JOSHUA MLERWA.
Kampuni ya Come and see Promoters inawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuwaenzi waimbaji wetu wakongwe ambao wengi wao ni wachungaji kwa sasa.
Subscribe to:
Posts (Atom)