COME AND SEE ANIMATED HEADER

WIMBO WA UPENDO NKONE WA HALELUYA AKIWA COLUMBUS U.S.A

Monday, October 22, 2012

COME AND SEE PROMOTERS TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUZINDUA BLOGU YETU JANA

Come and See Promoters tunamshukuru Mungu kwa wema wake kwa kutuwezesha kuzindua blogu yetu siku ya jana katika kanisa la TAG Magomeni hapa jijini Dar es Salaam. Pia tumshukuru mgeni rasmi mchungaji John na Mtangazaji wa TBC1 Jerry Muro kwa mchango wao mkubwa, na bila kuwasahau waimbaji wote waliofanya kazi kubwa sana katika kumtukuza Mungu kwa nia ya uimbaji. Wadau wangu mmekuwa msaada mkubwa sana kwa huduma yenu na kupoteza muda wenu kuja kunitia moyo.

Mkurugenzi wa RumaAfrica, Rulea Sanga umekuwa msaada kwangu kwa kufanikisha zoezi hili zima, tunautambua mchango wako wa kuitengeneza blogu hii ya www.comeandseemusic.blogspot.com..

MUNGU AWABARIKI

Mchungaji akihubiri kabla ya uzinduzi kuanza
Waimbaji wakimsindikiza mmbeba maono wa Come and See Promoter kwa uimbaji

Waimbaji wa Masengers Band
 Mmiliki wa blogu ya Come and See Promoter, Hima (kushoto) akipokea mchango kutoka kwa wadau wake
 Mgeni rasmi Mchungaji John wa tatu kutoka kulia akimkabidhi mic mmoja wa wadau ili atoe mchango wake kwaajili ya blogu
Mwimbaji wa nyimbo za injili akiahidi mchango kwaajili ya blogu
Mchungaji Sulley kulia akitoa ahadi yake kwaajili ya kuchangia blogu
  Jerry Murro akisoma Neno kwaajili ya kuhamasisha watu wachangie blogu
Blogu ikiwa katika projector

Blogu ikizinduliwa na mgeni rasmi Mchungaji John
 Jerry Muro wa pili kutoka kushoto akisikiliza hotuba kutoka kwa mubeba maono wa Come and See Promoters

Mwimbaji wa nyimbo za injili Madam Ruti wa Jana Imepita akimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji

Kutoka kulia ni Chris, MC Chavala na Madam Ruti wakiwa stejini

Saturday, October 20, 2012

BLOG YA WWW.COMEANDSEEMUSIC.BLOGSPOT.COM KUZINDULIWA LEO

Tunawashukuru Watanzania na watu wote mliofika katika uzinduzi huu wa blogu yetu mpya inayojihusisha na taarifa za waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Ndani ya blogu utajua kufahamu kazi mbalimbali za wasanii, matamsha yao, misafara yao nje ya Tanzania, mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari na mengine mengi.

UNAJUA MTUME NA NABII JOHN SIMON KOMANYA ANAIMBA NA KUMILIKI BAD YA JOY BAND

Mtume na Nabii John Simoni Komanya wa kanisa la furaha "Cathedral of Joy" ambaye anajulikana sana kwa nyimbo yake ya "Zawadi Gani Mimi Nitamtolea Bwana Wangu..." kwa sasa ana Band inayoitwa JOY Band inayofanya vizuri sana katika kazi ya Mungu.

Mtume John Simon Komanya akiwa na baadhi ya viongozi katika huduma ya Cathedral of Joy wakibariki waumini

 Mtume John Simon Komanya katikati akiwa na mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku kushoto na mchezaji wa Bukuku

Cathedral Joy Band wakiwa katika uimbaji. Kutoka kushoto ni Boniface Kachale, George Barnabas, Chillchala, Mhando Mkomwa, Peter Chikoga, Rehema


MADAM RUT KUWASHA MOTO KATIKA KANISA LA KKKT KARIAKOO

PURE MISSION KUWAKA IRINGA

WASANII WA NYIMBO INJILI TANZANIA

Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambao uimbaji wao umekuwa na faraja ndani ya mioyo ya watu. Mungu amewapa karama hiyo ya uimbaji ili kuokoa roho za watu na kuwaleta watu kwa Mungu. 
Pia kazi yao kubwa ni kumtukuza Mungu kwa njia ya sifa.
Christina shusho
Upendo Kilahiro(kulia) na Upendo Nkone (kushto)
Upendo Kilahiro akiwa na wapenzi wake jukwaani

Kutoka kulia ni Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Upendo Kilahiro (Tanzania), Upendo Nkone (Tanzania) wakiwa katikavyumba vya VIP uwanja wa Taifa kipindi cha Pasaka katika tamasha la Msama Promotion
Kushoto ni Upendo Nkone katika tamasha la Msama Promotion katika uwanja wa Taifa.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili na Mchungaji mtarajiwa Masanaja Mkandamizaji

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku

Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mtangazaji wa Praise Power, Victor Aloni

Mwimbaji wa nyimbo za injili, Rose Mhando


Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bony Mwaitege

SHIRIKIANA NA ROSE MHANDO KUIMBA WIMBO WA "NDIVYO ULIVYO"



BONYEZA HAPA KUONA ALICHOKIIMBA


BETI YA KWANZA

Naona kama maono, kumbe ndivyo ulivyo  Mkuu
Naona kama maono, kumbe ndivyo ulivyo  ooooh
Nilidhani kama ndoto, kumbe ndivyo ulivyo

Nilifikiri nachanganyikiwa kwa kusema hivi, kumbe ndivyo ulivyo ooh
Umekuwa mpole, umekuwa mwenye huruma, kumbe ndivyo ulivyo ooh

Simwepesi wa hasira, Baba ni mwingi wa rehema, ndivyo ulivyo ooh

Wewe, unatuwazia mema, kuliko tunavyodhani, ndivyo ulivyo ooh
Mawazo Yako hayafanani na mawazo ya wanadamu, Baba,  ndivyo ulivyo ooh

Nani kama Wewe,  mwepesi wa kusamehe, ndivyo ulivyo ooh
Wema wako haueleweke katikati ya wanadama Jehova, wewe,  kumbe ndivyo ulivyo ooh
----------------------------------------------------------
KIITIKIO

ROSE Ndivyo ulivyo, Ndivyo ulivyo, Ndivyo ulivyo ooh  Hakuna kupinga

ROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo x2

ROSE: Ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Babaaa, hakuna kupinga
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Wewe Mungu wa amani
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Mungu wa mapenzi mema
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Baba oooohooo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE Babaa
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, Hakuna wa kupinga

ROSE: Wewe si mwepesi wa hasira
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Huangalii mabayaWAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Babaaa
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, hakuna kupinga

ROSE: Wewe unatuwazia mema
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo
ROSE: Babaaa oh
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: HaleluyaWAITIKIAJI: Ndivyo ulivyoROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo hakuna kupinga

ROSE: Nasema kumbe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyoROSE: Kumbe ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo
ROSE: BabaaaWAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, hakuna kupinga

--------------------------------------------

BETI YA PILI

Tulia kwa Mungu, hushuka na kutufariji
Baba, kumbe ndivyo ulivyo ooh

Usiku na mchana hulali usinzi
Mungu uliye hai, ndivyo ulivyo ooh

Pale, tusipoweza kutenda wenyewe kwa mikono yetu Yehova, ndivyo ulivyo ooh
Huingilia kati yale yote tunayoshindwa, wewe, ndivyo ulivyo ooh

Msaada wakati tunapochoka, Yeeeeehova, ndivyo ulivyo ooh
-------------------------------------------------------

KIITIKIO
ROSE: Ndivyo ulivyo ooh x3, Hakuna kupinga

ROSE: Wewe Umepanda milimani
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyoo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE:  aah..oooh
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, Hakuna kupinga

ROSE: Mungu wewe, mwenye mamlaka
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyo, Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: weweeee hee
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo hakuna kupinga

ROSE: Uliyeketi mahali pa juu
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Mungu Uliye hai
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Yeeehova ataishi
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, Hakuna kupinga

ROSE: Huhesabu mabaya yetu
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Wala hutazami dhambi zetu
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Babaaa oh
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo hakuna kupinga

ROSE: Nasema kumbeeee
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Kumbeee
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Kumbeee, ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyohakuna kupinga

ROSE: weweeeee
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyoo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Hakuna kupinga
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Oooh Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo hakuna kupinga

BETI YA TATU

Mungu,  uliwakusanya walioachwa,  ukawakumbatia, Baba,ndivyo ulivyo ooh
Waliokosa, tumaini, huweka tumaini jipya kwao, ndivyo ulivyo ooh

Waliokataa tamaa wewe unawatia nguvu, Baba, ndivyo ulivyo ooh
Vile nionavyo mimi, si kama wewe utazamavyo Baba, kumbe ndivyo ulivyo ooh

Huruma zako zimevuka vilindi vya bahari, Weweeeee eh, kumbe ndivyo ulivyo, hakuna kupinga
----------------------------------------------------------------
KIITIKIO
ROSE: Eeeeh
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Babaaaa eeh
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Baba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, hakuna wa kupinga

ROSE: Baba nakuinua Wewe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Nakuambudu wewe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Hivi ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Babaaa ahaa
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Nakushukuru Ulivyoniumba
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Umenikumbuka
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Kumbe ndivyo ulivyo
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, hakuna kupinga

ROSE Umenitete mbele ya wenye nguvu, Yehova
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyo,Baba yangu
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, hakuna kupinga

ROSE: Wacha nikuinue wewe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Wacha nikuabudu wewe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Ndivyo ulivyo, Babaa
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Wacha nikuinue wewe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Nisimulie matendo yako
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Babaaa
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Acha nikuimbie wewe
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Kwa sauti yangu
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Yehooovaaaa
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: ooooooohhhh
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo, hakuna kupinga

ROSE: yeeeeeeheeeee
WAITIKIAJI: Ndivyo ulivyo

ROSE: Wewe ndivyo ulivyo

MUNGU AKUBARIKI
Mwandishi: Rulea Sanga

LINKWITHIN

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...