COME AND SEE ANIMATED HEADER

WIMBO WA UPENDO NKONE WA HALELUYA AKIWA COLUMBUS U.S.A

Monday, October 22, 2012

COME AND SEE PROMOTERS TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUZINDUA BLOGU YETU JANA

Come and See Promoters tunamshukuru Mungu kwa wema wake kwa kutuwezesha kuzindua blogu yetu siku ya jana katika kanisa la TAG Magomeni hapa jijini Dar es Salaam. Pia tumshukuru mgeni rasmi mchungaji John na Mtangazaji wa TBC1 Jerry Muro kwa mchango wao mkubwa, na bila kuwasahau waimbaji wote waliofanya kazi kubwa sana katika kumtukuza Mungu kwa nia ya uimbaji. Wadau wangu mmekuwa msaada mkubwa sana kwa huduma yenu na kupoteza muda wenu kuja kunitia moyo.

Mkurugenzi wa RumaAfrica, Rulea Sanga umekuwa msaada kwangu kwa kufanikisha zoezi hili zima, tunautambua mchango wako wa kuitengeneza blogu hii ya www.comeandseemusic.blogspot.com..

MUNGU AWABARIKI

Mchungaji akihubiri kabla ya uzinduzi kuanza
Waimbaji wakimsindikiza mmbeba maono wa Come and See Promoter kwa uimbaji

Waimbaji wa Masengers Band
 Mmiliki wa blogu ya Come and See Promoter, Hima (kushoto) akipokea mchango kutoka kwa wadau wake
 Mgeni rasmi Mchungaji John wa tatu kutoka kulia akimkabidhi mic mmoja wa wadau ili atoe mchango wake kwaajili ya blogu
Mwimbaji wa nyimbo za injili akiahidi mchango kwaajili ya blogu
Mchungaji Sulley kulia akitoa ahadi yake kwaajili ya kuchangia blogu
  Jerry Murro akisoma Neno kwaajili ya kuhamasisha watu wachangie blogu
Blogu ikiwa katika projector

Blogu ikizinduliwa na mgeni rasmi Mchungaji John
 Jerry Muro wa pili kutoka kushoto akisikiliza hotuba kutoka kwa mubeba maono wa Come and See Promoters

Mwimbaji wa nyimbo za injili Madam Ruti wa Jana Imepita akimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji

Kutoka kulia ni Chris, MC Chavala na Madam Ruti wakiwa stejini

No comments:

Post a Comment

LINKWITHIN

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...