Kampuni ya COME AND SEE PROMOTERS imeandaa Tamasha kubwa la wakongwe wa muziki wa injili Tanzania kwa lengo la kutambua mchango mkubwa ambao wameutoa waimbaji hawa wazamani wa muziki wa injili katika kuinua na kuendeleza mziki wa injili Tanzania. Akiongea kwa nyakati tofauti mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Come and see Promoters bwana Emmanuel Ezekiel ( Pastor Pepea ) Amesema hili ni tamasha la kihistori ambapo halijawahi kutokea katika nchi yetu ambapo waimbaji wote wakongwe wa mziki wa injili kukutana katika jukwaa moja.Tamasha hili limepewa jina la OLD IS GOLD DAY linatarajia kufanyika tarehe 17/3/2013 katika ukumbi mtulivu wa Diamond Jubilee kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni na kukusanya wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikari,viongozi wa dini, waandishi wa habali nk.
Tamasha hili litaambatana na utoaji wa Tuzo za heshima kwa waimbaji hawa wakongwe ili kutambua mchago wao katika kuinua na kuendeleza wa injili Tanzania. Waimbaji wakongwe wa mziki wa injili watakaoshambulia jukwaa ni MZUNGU FOUR, JANGARASONI, MASAGA NYANDA,DAVIDI NKONE, NATHANIEL HINGI, MWASASU, MWASUMBI, ENCY MWALUKASA, AMON NA UPENDO KIRAHIRO, NEW LIFE BAND TOKA ARUSHA, na kwa upande wa kwa ya ni LULU KWAYA NAYOTH KWAYA ,VICTORY SINGERS , MSASANI KWAYA NK na kusindikizwa na JOSHUA MLERWA.
Kampuni ya Come and see Promoters inawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuwaenzi waimbaji wetu wakongwe ambao wengi wao ni wachungaji kwa sasa.
No comments:
Post a Comment