Come and See Promoters tunamshukuru Mungu kwa wema wake kwa kutuwezesha kuzindua blogu yetu siku ya jana katika kanisa la TAG Magomeni hapa jijini Dar es Salaam. Pia tumshukuru mgeni rasmi mchungaji John na Mtangazaji wa TBC1 Jerry Muro kwa mchango wao mkubwa, na bila kuwasahau waimbaji wote waliofanya kazi kubwa sana katika kumtukuza Mungu kwa nia ya uimbaji. Wadau wangu mmekuwa msaada mkubwa sana kwa huduma yenu na kupoteza muda wenu kuja kunitia moyo.
Mkurugenzi wa RumaAfrica, Rulea Sanga umekuwa msaada kwangu kwa kufanikisha zoezi hili zima, tunautambua mchango wako wa kuitengeneza blogu hii ya www.comeandseemusic.blogspot.com..
MUNGU AWABARIKI
Mchungaji akihubiri kabla ya uzinduzi kuanza
Waimbaji wakimsindikiza mmbeba maono wa Come and See Promoter kwa uimbaji
Waimbaji wa Masengers Band
Mmiliki wa blogu ya Come and See Promoter, Hima (kushoto) akipokea mchango kutoka kwa wadau wake
Mgeni rasmi Mchungaji John wa tatu kutoka kulia akimkabidhi mic mmoja wa wadau ili atoe mchango wake kwaajili ya blogu
Mwimbaji wa nyimbo za injili akiahidi mchango kwaajili ya blogu
Mchungaji Sulley kulia akitoa ahadi yake kwaajili ya kuchangia blogu
Jerry Murro akisoma Neno kwaajili ya kuhamasisha watu wachangie blogu
Blogu ikiwa katika projector
Blogu ikizinduliwa na mgeni rasmi Mchungaji John
Jerry Muro wa pili kutoka kushoto akisikiliza hotuba kutoka kwa mubeba maono wa Come and See Promoters
Mwimbaji wa nyimbo za injili Madam Ruti wa Jana Imepita akimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji
Kutoka kulia ni Chris, MC Chavala na Madam Ruti wakiwa stejini
Tunawashukuru Watanzania na watu wote mliofika katika uzinduzi huu wa blogu yetu mpya inayojihusisha na taarifa za waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania. Ndani ya blogu utajua kufahamu kazi mbalimbali za wasanii, matamsha yao, misafara yao nje ya Tanzania, mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari na mengine mengi.
Mtume na Nabii John Simoni Komanya wa kanisa la furaha "Cathedral of Joy" ambaye anajulikana sana kwa nyimbo yake ya "Zawadi Gani Mimi Nitamtolea Bwana Wangu..." kwa sasa ana Band inayoitwa JOY Band inayofanya vizuri sana katika kazi ya Mungu.
Mtume John Simon Komanya akiwa na baadhi ya viongozi katika huduma ya Cathedral of Joy wakibariki waumini
Mtume John Simon Komanya katikati akiwa na mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku kushoto na mchezaji wa Bukuku
Cathedral Joy Band wakiwa katika uimbaji. Kutoka kushoto ni Boniface
Kachale, George Barnabas, Chillchala, Mhando Mkomwa, Peter Chikoga,
Rehema
Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambao uimbaji wao umekuwa na faraja ndani ya mioyo ya watu. Mungu amewapa karama hiyo ya uimbaji ili kuokoa roho za watu na kuwaleta watu kwa Mungu.
Pia kazi yao kubwa ni kumtukuza Mungu kwa njia ya sifa.
Christina shusho
Upendo Kilahiro(kulia) na Upendo Nkone (kushto)
Upendo Kilahiro akiwa na wapenzi wake jukwaani
Kutoka kulia ni Ephraim Sekeleti kutoka Zambia, Upendo Kilahiro (Tanzania), Upendo Nkone (Tanzania) wakiwa katikavyumba vya VIP uwanja wa Taifa kipindi cha Pasaka katika tamasha la Msama Promotion
Kushoto ni Upendo Nkone katika tamasha la Msama Promotion katika uwanja wa Taifa.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili na Mchungaji mtarajiwa Masanaja Mkandamizaji
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku
Mwimbaji wa nyimbo za Injili na mtangazaji wa Praise Power, Victor Aloni